HERI YA MWAKA MPYAA Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru wewe mpenzi mfuatiliaji wa nakala mbali mbali zinazokuja na lengo la kuelimisha jamii kuhusu lishe bora kwa ajili yako na familia yako. AfyaLishe Tz inakuletea zawadi ya mwaka mpya kwa kufungua kurasa mpya itakayokuja kwa jina la JengaFamilia . Jenga familia inakuja kwako kukuelimisha maswala mbali mbali kuhusu familia kama msingi wa kila kitu. Katika kurasa hii utakutana na nakala mbali mbali zitakazokujuza ujenge vipi familia yako ili kuboresha maendeleo katika jamii nzima inayokuzunguka, lakini pia itakupa uzoefu mbali mbali utakaokufanya ufahamu jinsi ya kuwa na amani katika maisha yako. Kurasa hii pia inakuja na huduma ya counselling/ ushauri ambapo hapa utapata fursa ya kuachilia mambo mbali mbali yanayokutatiza katika maisha yako na hakika utapata faraja baada ya kusikilizwa, na utapata ushauri kutoka kwa mtaalamu wetu wa maswala ya kijamii na familia, Ms Sylvia Senkoro, Mkurugenzi mtendaji wa AfyaLishe bl...