Maziwa ya Soya Aina hii ni maarufu pia, na kwa kuwa yanatokana na mimea, maziwa haya hana cholesterol ( lehemu) - tofauti na maziwa ya kawaida. Maziwa ya Soya pia yana kiwango cha chini cha kalori kuliko maziwa ya ng'ombe, yana kalori takribani 130 kwa kila kikombe. Hakuna lactose katika maziwa haya, aina ya protini inayoleta sana gesi tumboni, hivyo huyafanya kuwa mbadala muhimu kwa watu ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa kushindwa kuvumilia lactose (lactose intolerance) katika mfumo wao wa umeng'enyaji, pamoja na watu wasiotumia bidhaa zitokanazo na wanyama pia (vegeterians) sababu haitoki kwa wanyama. Soya ni mboga nzuri sana, na maziwa yanayotokana na jamii hii yana utajiri wa potasiamu, protini na kalsiamu ikiwa mtengenezaji atayaimarisha na madini. Pia ni chanzo kikubwa cha vitamini A na vitamini B12, ambayo haipo katika aina nyingine za maziwa. Maziwa ya Soya hutoa kiwango cha juu cha protini, pia ni bora kwa watu ambao wanajaribu kudhibiti uzito wao au kupu...