UANDAAJI WA LISHE YA UJI UNAOTAKIWA KWA MTOTO MIEZI SITA NA KUENDELEA
Tumekua na tamaduni ya kuandaa uji wa lishe ya mtoto bila kufuata kanuni za uandaaji bora.
Madhara ya uji usio bora
📌Kusababisha magonjwa
📌Unenepaji usiofaa
Uandaaji bora wa uji lishe kwa mtoto
🏮Kitu cha msingi cha kuzingatia ni kuandaa uji utaoweza kumpatia mtoto virutubisho anavyohitaji kwa umri wake ili kusaidia ukuaji na maendeleo bora kwa afya ya mtoto.
📌Virutubisho muhimu zaidi kwa mtoto ni
🏮Wanga
Kuupa mwili nguvu
Mahindi/Mchele/Viazi n.k
🏮Protini
Hujenga mwili
Soya/Maharage n.k
🏮Mafuta
Kutia joto
Ufuta/Karanga n.k
Zingatia katika uandaaji
📌Tumia aina moja ya nafaka kwa kila kirutubishi.
🍲Kwanini?
Kila nafaka inakiwango chake cha uivaji, kutumia nafaka zaidi ya moja kwa ajili ya kupata kirutubishi husika ni hatari, maana: vinapo tofautiana kuiva kunaweza sababisha maumivu ya tumbo na magonjwa mengine kwa mtoto.
📌 uwiano sahihi wa vyanzo vya nafaka.
Kwanini?
Kiwango cha virubishi anavyohitaji mtoto hutofautiana kulingana na mahitaji ya ukuaji na maendeleo ya mtoto
📌Uchanganyaji na uandaaji vyanzo virutubishe uwe katika hali ya usafi ili kuepuka magonjwa.
Uandaaji
🍲zingatia mahitaji
Formula ya mfano
🍲Mahitaji
🌽Mahindi ya njano - chanzo cha wanga
🌽Soya - chanzo cha protini
🌽Ufuta - chanzo cha mafuta
🍲Uwiano
🌽Chanzo cha Wanga kilo moja-1kg
🌽Chanzo cha Protini nusu kilo-1/2 kg
🌽Chanzo cha Mafuta robo kilo-1/4 kg
🍲Uchanganyaji
🌽osha mahindi, soya, ufuta vizuri kila moja pekeake baada ya kuvichambua.
🌽Anika juani hakikisha vumbi halitaingia.
🌽Changanya vyanzo vyako na kisha saga.
🌽Unga tayari kwa matumizi.
MUHIMU
Uandaaji wa soya
🏮Ni muhimu kuhakikisha umetoa maganda ya soya vizuri maana katika ganda kuna aina ya kirutubishi kinachozuia unyonywaji wa kirutubisho cha protini katika mwili wa mtoto baada ya umeng'enyaji chakula.
Matumizi ya karanga
🏮 kama utatumia karanga katika usagaji, iandae na kuisaga peke yake na uichanganyie wakati wa kupika uji.
🍲Karanga huwai kuchacha joto likiongezeka ndio maana tunaiandaa pembeni na kuichanganyia wakati wa kupika ili kuweza kukinga kuchachisha na nafaka zingine ambapo kukitokea kutamletea madhara mtoto kama kuharisha.
🍲Karanga itumike ndani ya siku saba tu baada ya kusagwa maana baada ya hapo itakua imeshachacha.
🏮 Muda wa kupika uji
🍲Katika kupika uji wa mtoto hakikisha unapika uji kwa muda usiopungua nusu saa mpaka dakika 45 ili kuhakikisha kua umeiva vizuri.
🏮 kiwango cha virutubisho bora katika vaadhi ya nafaka
🍲Utumiaji wa mahindi ya njano au viazi vya njano kama chanzo cha wanga ni bora zaidi kwamaana vina kiwango kikubwa cha vitamini A, hii humsaidia mtoto katika :
🍲Kuimarisha macho yake
By Sylvia Senkoro
AfyaLishe Tz
0754031039/0655568468
sylsenkoro@gmail.com
afyalishetz@gmail.com
shukran
ReplyDeleteshukran
ReplyDeleteAsante sana. Naomba kufahamu karanga ni bora kuzikaanga kabla ya kusaga?
ReplyDeleteAsante nimejifunza
ReplyDeleteNaomba nijue mwanangu bado hajatimiza miezi sita je atakapoa Anza tu Kula naweza kumuanzisha lishe moja kwa moja
ReplyDeleteUnaweza kuanza lishe ila inatakiwa kuwa ni nyepesi na kidogo, unaanza kidogo kidogo hadi anazoea.
DeleteTofauti ya soya na soya maziwa n nn? Na naruhusiwa kutumia soya maziwa?
DeleteVipi mtoto wa miaka mitano soya yake naweza iacha na maganda?
ReplyDeleteHahaha ww kavivu kuandaa soya ee hahah
DeleteZipo soya ambazo teali zimeshakobolewa yaani zimeshatolewa maganda na unapata kwenye maduka ya nafaka
DeleteWapi hizo zapatikana mbona hatuzioni masokoni
DeleteAsante Sana Kwa elim nzuri nikitumia mbegu za maboga ktk mchanganyiko badala ya Karanga inafa na pia naruhudiwa kisaga pamoja au nayo nisage pembeni kama Karanga ulivyosema tusichanye mana huchacha
DeleteAsante kwa kutoa elimu nzuri
ReplyDeleteShukran ana
ReplyDeleteAhsanten sana kwa elimu Nzur
ReplyDeleteHii garage soya walitoa vipi maganda
ReplyDeletenimejifunza
ReplyDeleteNaomba kujua ni nafaka gani zinazotakiwa kukaangwa kabla ya kuzisaga tofauti na karanga?
ReplyDeleteTushukuru sana kwa somo lenye maelekezo mazuri.
DeleteNaomba kujua mtoto wa miezi sita anafaa kunywa uji wa lishe uliochanganywa na nafaka zaidi ya tatu?
Duh nimejifunza lkn hy soya jmn kuiandaa Ni kazi Lkn km unahtj mtt awe na lishe nzr Ni Bora kuiweka
ReplyDeleteNa nikazi kweli huwa inachukua hata siku nzima ila kwa afya ya mtoto ni bora kuandaa tu
DeleteAhsante kwa somo zuri..
ReplyDeleteBARIKIWA
asante kwa somo zuri
ReplyDeleteSomo zuri
ReplyDeleteAsante Kwa elimu nzuri
ReplyDeleteShukrani
ReplyDeleteAsante sanaaz ila naomba kujuaa naweza kumuekea almond badala ya karanga
ReplyDeleteNashkru kwa somo zuri Sana, barikiwa
ReplyDeleteAsanteee sana kumbe mm huwa nakosea namwekea mtt mavitu mengi mwili ata hauji raund hii nasaga kwa maelezo yako
ReplyDeleteNatamani kueleweshwa juu ya siku 1000 za mtoto
ReplyDeleteNaomba kuna ukikosa soya waweza tumia nn
ReplyDeleteAhsante
ReplyDeleteMwanangu anapata choo kigumu nisaidiwe nifanyeje
DeleteMbegu za maboga naweza tumia badala ya soya au husaidia nini kwenye lishe
ReplyDeleteMnegu za maboga zina madini ya zinc kwa wingi kama n wa kiume basi hatakuja kupata shida ya nguvu za kiume
DeleteNa vipi ukitumia almond kama chanzo cha protein?
ReplyDeleteJe mtoto mwenye afya njema anatakiwa kudumu kwenye lishe ya uji kwa muda gani kabla ya kuingia lishe ya vyakula vya kupondaponda? Vipi kwa mtoto mwenye maradhi ya mara kwa mara au mtoto mwenye changamoto ya ulemavu hususani ulemavu wa viungo?
ReplyDeleteAsante sana kwa elimu hii nzuri kwa Jamii. Mungu akubariki sana.
ReplyDeleteJe nikishaundaa huo unga wakati wa kuupika naweza kuuchuja au nipike hivyo
ReplyDelete