Skip to main content
""Kwa msaaada zaidi wasiliana nasi kwa namba zifuatazo 0754031039/0655568468 AfyaLishe Tz kwa ajili yako""

COUNSELLING DESK

COUNSELLING DESK
Tumia huduma yetu ya ushauri, na kujadiliana. Kwa matatizo ya kifamilia, kibiashara, kielimu, kiafya, mahusiano na mfumo mzima wa maisha wasiliana nasi kwa 0754031039 au 0655568468

ONGEZA UWEZO WAKO WA KUMNYONYESHA MTOTO

ONGEZA UWEZO WAKO WA KUMNYONYESHA MTOTO

Mtoto anyonye maziwa ya mama tu hadi ayakapotimiza Miezi sita.
Utakua umemuepushia magonjwa na hatari zingine nyingi tu.

Kama mama hana maziwa ya kutosha mtoto pia anaweza kupewa formula milk ila ni pale tu mama akiwa maefariki au akiwa na tatizo kama hilo la maziwa kuto tosha.

Lakini ni muhimu mama kukazana kuhakikisha maziwa yanatosha ili mtoto awe katika hali salama na afya zaidi.

Fahamu vitu vifuatavyo vimesaidia wengine

🍵Maziwa ya mama yametengenezwa na vtu vi3 vya muhimu

*maji ambayo ndio mengi
*Protein and
*Fats

🍵 ni muhimu sana kufahamu kwamba  kutoka kwa  Maziwa kunahitaji activity ya hormones/ homoni ziwe stimulated, na kinachostimulate ni mtoto kunyonya au kuvuta chuchu
Hivyo mtoto anavovuta au kunyonya chuchu ya mama yake ndivo hormones za kutengeneza  maziwa zinavozalishwa zaidi, hivyo kuleta matokeo chanya katika unyonyeshaji.

Mama asikate tamaa kumueka mtoto kwenye chuchu hata kama maziwa hayatoki auni machache maana kutasaidia kuzalisha homoni zitakazosaidia kutatua tatizo la maziwa kutotosha.

MLO WA MAMA ANAYENYONYESHA

🍵kupata maji ya kutosha au vyakula vya kimiminika, starch/ wanga (mahindi, viazi
,  ndizi) ya kiasi, protein ( jamii ya kunde, maharage, soya na nyama vyakula vitokanavyo na wanyama) na mafuta ( karanga, mlozi au almond  mbegu za maboga, korosho).

Bila kusahau vyakula vya vitamins and minerals/madini kwa kiasi. (matunda na mboga mboga)

Yaani mlo kamili.

🍵Muweke pia mtoto kwenye chuchu hata kama maziwa hakuna mara kwa mara hii itasaidia uzalishaji wa maziwa.
Ndio mana mama anapotaka kumuachisha mtoto nyonyo hua hampi na maziwa yanakata automatically
So zingatia hilo ikiwezekana uweke timetable ya kufanya hyo therapy kabisa.

🍵La mwisho some recipes/vyakula ambavyo vitakusaidia

*uwatu / fenugreek
Loweka na chemshia kisha kunywa maji yake ya kiwa ya moto au baridi, unaweza weka asali kuongeza ladha.

*Unga wa  mlonge, tumia kama kiungo kwenye vyakula vyako, nyunyizia kijiko full cha chakula on a plate with ready to eat food.
*Pilipili manga kwenye uji anaokunywa mzazi au mtori au chai.
*Mbegu za maboga kama kiungo kwenye chakula au uji unavyopika.

*Maji tena nazidi kuwekea mkazo.

Sample diet
From one of my clients and imemsaidia, sahivi ana maziwa ya kutosha na si yeye tu hadi wamama wengi.
Mwanzoni hakuwa na maziwa ya kutosha kabisa.

Routine ya kula yenye kuonyesha jinsi utakavyoingizia hzo recepies za kuingeza maziwa kwenye milo yako ya kila siku.

12 asubuh (oat+maziwa+unga wa maboga+ tende) na glass ya maji ya uwatu
2 asubuh chai yako kama kawaida

4 asubuh uji changanya na unga wa maboga + glass ya uwatu

6 /7 lunch yako iwe na protein ya kutosha + glass ya uwatu

Saa 10 maziwa + tende 10

Saa 1/2 ucku dinner na glasss ya uwatu

Saa 4 ucku , saa 6 na saa 9 ucku  either of these, oats+ maziwa+ unga wa maboga+ uwatu.

ZINGATIA
Mama wengi wanaonyonyeaha wanapata stress za kunenepa kupitiliza hivo hawali kama inavotakiwa au wanakua mislead wanakula mno na kujijazia excess mwilini na baadae kujichukia bcoz of mwili kujiachia bila mpangilio.

Kula sana si kupata maziwa mengi. Unatakiwa kula mlo uliokamili na kujitahidi kunyonyesha mtoto wako.

Fanya mazoezi simple ili kuweka mwili wako active na kuzuia unene bila mpangilio.

By
ReSta Dietetics & Counselling
0754031039
afyalishetz.blogspot.com

Comments

Post a Comment

NEWS

NEWS
Kula lishe bora kuepuka hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa.

Chagua afya leo.

EXCLUSIVE BREASTFEEDING

EXCLUSIVE BREASTFEEDING
Make sure your child gets breastfed exclussively for the first six months, the child shouod not be fed anything else not even water. This adds up to the child's immunity and increase chencea of proper development.

Popular posts from this blog

UANDAAJI WA LISHE YA UJI UNAOTAKIWA KWA MTOTO MIEZI SITA NA KUENDELEA

UANDAAJI WA LISHE YA UJI UNAOTAKIWA KWA MTOTO MIEZI SITA NA KUENDELEA Tumekua na tamaduni ya kuandaa uji wa lishe ya mtoto bila kufuata kanuni za uandaaji bora. Madhara ya uji usio bora

KANUNI BORA ZA KUMUANZISHIA MTOTO CHAKULA AFIKAPO MIEZI SITA

KANUNI BORA ZA KUMUANZISHIA MTOTO CHAKULA AFIKAPO MIEZI SITA 🏮 Kwanini nianze kumpa mtoto wa miezi 6 chakula kingine? 🍲Mtoto wa miezi sita ameanza kuwa na mahitaji ya virutubishi  kwa wingi zaidi ya anavyopata kutoka kwenye maziwa ya mama.
""AHSANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU, KARIBU TENA/ THANK YOU FOR VISITING OUR BLOG, YOU ARE WELCOME""