Skip to main content
""Kwa msaaada zaidi wasiliana nasi kwa namba zifuatazo 0754031039/0655568468 AfyaLishe Tz kwa ajili yako""

COUNSELLING DESK

COUNSELLING DESK
Tumia huduma yetu ya ushauri, na kujadiliana. Kwa matatizo ya kifamilia, kibiashara, kielimu, kiafya, mahusiano na mfumo mzima wa maisha wasiliana nasi kwa 0754031039 au 0655568468

FAHAMU CHAKULA BORA KWA MTOTO ANAEPATA KIDOGO AU ASIEPATA KABISA MAZIWA YA MAMA.

FAHAMU CHAKULA BORA KWA MTOTO ANAEPATA KIDOGO AU  ASIEPATA KABISA MAZIWA YA MAMA.
(Umri 0- miezi 6)




🏮 Mtoto anapozaliwa hutakiwa kupata maziwa ya mama ndani ya lisaa tu baada ya kuzaliwa, lakini

Kutokana na matatizo mbali mbali ya uzazi watoto wengine hawawezi kupata chakula hiki muhimu na kuongezeka kwa uwezekano wa wao kuwa na lishe duni


🏮hii ni hatari maana muda huu ni muhimu kujenga mwili na mifumo mbali mbali muhimu ya mtoto.

🏮Epusha udumavu wa akili, mwili na maendeleo mengine ya mtoto wako kwa kumyonyesha vizuri tangu anavyozaliwa hadi afikishapo miezi sita bila kumpa kitu chochote hata maji

🌽Sina maziwa ya kutosha nifanyaje?
🌽Mama mzazi amefariki mtoto ale nini?
Na mengineyo ni baadhi ya maswali walezi wengi wamekua wakijiukiza

🏮 SULUHISHO

Mtoto anaweza pewa vyakula vifuatavyo;

🌽Formula za maziwa zilizotengenezwa viwandani.
Hupatikana madukani.

📌Formula hizi huwa zimeandaliwa vizuri na mfumo wa mtoto huweza kupokea chakula hiki.
🌽Maziwa ya ng'ombe
Maziwa haya huandaliwa kwa utaalamu ili mfumo wa kumeng'enya chakula wa mtoto uweze kuyapokea bila kumletea mtoto athari zozote.
🌽 Formula ya uji wa lishe.
Uji huu pia huandaliwa kwa njia maalumu , ili kumwezesha mtoto kupokea bila madhara.

Makala hii itaeleza zaidi juu ya utayarishaji wa uji huu muhimu, Mbadala wa maziwa ya mama

🏮 Mahitaji

🌽Maziwa fresh bora- nusu lita1/2L
🌽Maji safi  - nusu lita 1/2 L
🌽Chanzo cha wanga kimoja ( udaga/ unga wa mahindi/ unga wa viazi vya njano lishe) - 40g vijiko vinne vya chakula
🌽Sukari - 30g vijiko vitatu cya chakula.
🌽Chumvi - 10g kijiko kimoja cha chakula.

🏮 Uandaaji

🌽Chukua maziwa fresh nusu lita chuja kuhakikisha yanatoa uchafu au uzito wowote uliopo na usiofaa, kisha weka kwenye chombo safi.
🌽Andaa maji safi vizuri kwa kutachemsha kisha yaache yapoe,
🌽Chuja na pima kiasi cha nusu lita, kisha hifadhi maji yaliyobaki kwenye chombo safi pembeni kwa matumizi ya baadae.
🌽Changanya maji nusu lita na maziwa nusu lita yalioandaliwa vizuri kama ilivyoelekezwa hapo juu.
🌽Fuata kuandaa chanzo cha wanga,  Chukua unga wako wa mahindi ya njano kipimo elekezi pale juu sawa na vijiko 4 vya chakula.
🌽chekecha unga wako hakikisha hauna mabonge bonge.
🌽weka unga wako ndanibya kikombe chenye ujazo wa nusu lita.
🌽Chukua maji salama uliyohifadhi awali na mimina ndani ya kikombe ulichoweka unga, mimina hadi kukamilisha kipimo cha nusu lita kwenye kikombe.
🌽changanya mchanganyiko wako vizuri kwa kukoroga.

🏮 Upikaji

🌽Andaa jiko liwake vizuri.
🌽Weka sufuria jikoni, mimina mchanganyiko wa kwanza wenye maji na maziwa, kisha weka mchanganyiko wa pili  wenye maji na unga huku ukikoroga vizuri.
🌽Endelea kukoroga unga usituame chini hadi utakaposhikana  vizuri.
🌽Mchanganyiko wako Unapoendelea kuiva weka vijiko vitatu vya sukari safi na kijiko kimoja cha chumvi safi  kwenye uji unaoiva.
🌽Koroga vizuri vichanganyike.
🌽Acha uji uive vizur.
🌽Unashauriwa kupika uji kwa muda wa nusu saa hadi dakika 45 kwa uhakika wa kuivisha uji vizuri.
🌽Hakikisha uji umeiva vizuri , Zingatia uzito usiwe mkubwa sana hasa kwa mtoto mdogo zaidi.
🌽Ongeza maji safi yalioandaliwa awali kama uzito ukizidi kidogo kidogo ukikoroga vizuri ili kuweka uzito wa uji sawa.
🌽Tunza uji wako kwenye chupa yenye uwezo wa kutunza joto  safi.
🌽Tayari kwa kumpa mtoto.

🏮 MUHIMU
🌽 kwa mtoto asiepata maziwa ya mama kabisa apewe uji huu ndani ya miezi sita peke yake bila kitu chochote kingine.
🌽kwa mama anaenyonyesha kidogo, amuongezee mtoto uji huu kama chakula cha pili, bila kumpa mtoto kingine chochote.


🏮 Kiasi cha kumlisha mtoto kwa umri husika

🌽0-1
Milo 8 kwa siku.
60 mls kwa kila mlo

🌽1-2
Milo 7 kwa siku.
90 mls kwa kila mlo

🌽2-4
Milo 6 kwa siku.
120 mls kwa kila mlo

🌽4_6
Milo 6 kwa siku.
120 mls kwa kila mlo

MUHIMU
🏮Mtoto apewe mlo huu tu ndani ya miezi sita.
Utampatia virutubisho bora  anavyohitaji kwa ajili ya ukuaji wake.

🏮Chakula hiki pia hupewa wagonjwa wa utapiamlo,
Huwasaidia kutengemaza afya zao taratibu.

By  Sylvia Senkoro
AfyaLisheTz
0754031039
0655568468
sylsenkoro@gmail.com
afyalishetz.blogspot.com

Comments

NEWS

NEWS
Kula lishe bora kuepuka hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa.

Chagua afya leo.

EXCLUSIVE BREASTFEEDING

EXCLUSIVE BREASTFEEDING
Make sure your child gets breastfed exclussively for the first six months, the child shouod not be fed anything else not even water. This adds up to the child's immunity and increase chencea of proper development.

Popular posts from this blog

UANDAAJI WA LISHE YA UJI UNAOTAKIWA KWA MTOTO MIEZI SITA NA KUENDELEA

UANDAAJI WA LISHE YA UJI UNAOTAKIWA KWA MTOTO MIEZI SITA NA KUENDELEA Tumekua na tamaduni ya kuandaa uji wa lishe ya mtoto bila kufuata kanuni za uandaaji bora. Madhara ya uji usio bora

KANUNI BORA ZA KUMUANZISHIA MTOTO CHAKULA AFIKAPO MIEZI SITA

KANUNI BORA ZA KUMUANZISHIA MTOTO CHAKULA AFIKAPO MIEZI SITA 🏮 Kwanini nianze kumpa mtoto wa miezi 6 chakula kingine? 🍲Mtoto wa miezi sita ameanza kuwa na mahitaji ya virutubishi  kwa wingi zaidi ya anavyopata kutoka kwenye maziwa ya mama.

ONGEZA UWEZO WAKO WA KUMNYONYESHA MTOTO

ONGEZA UWEZO WAKO WA KUMNYONYESHA MTOTO Mtoto anyonye maziwa ya mama tu hadi ayakapotimiza Miezi sita. Utakua umemuepushia magonjwa na hatari zingine nyingi tu. Kama mama hana maziwa ya kutosha mtoto pia anaweza kupewa formula milk ila ni pale tu mama akiwa maefariki au akiwa na tatizo kama hilo la maziwa kuto tosha. Lakini ni muhimu mama kukazana kuhakikisha maziwa yanatosha ili mtoto awe katika hali salama na afya zaidi. Fahamu vitu vifuatavyo vimesaidia wengine 🍵Maziwa ya mama yametengenezwa na vtu vi3 vya muhimu *maji ambayo ndio mengi *Protein and *Fats 🍵 ni muhimu sana kufahamu kwamba  kutoka kwa  Maziwa kunahitaji activity ya hormones/ homoni ziwe stimulated, na kinachostimulate ni mtoto kunyonya au kuvuta chuchu Hivyo mtoto anavovuta au kunyonya chuchu ya mama yake ndivo hormones za kutengeneza  maziwa zinavozalishwa zaidi, hivyo kuleta matokeo chanya katika unyonyeshaji. Mama asikate tamaa kumueka mtoto kwenye chuchu hata kama maziwa hayatoki auni macha
""AHSANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU, KARIBU TENA/ THANK YOU FOR VISITING OUR BLOG, YOU ARE WELCOME""