KANUNI BORA ZA KUMUANZISHIA MTOTO CHAKULA AFIKAPO MIEZI SITA
🏮 Kwanini nianze kumpa mtoto wa miezi 6 chakula kingine?
🍲Mtoto wa miezi sita ameanza kuwa na mahitaji ya virutubishi kwa wingi zaidi ya anavyopata kutoka kwenye maziwa ya mama.
🍲Mfumo wake wa mwili unaruhusu upokeaji.
🍲 Si rahisi kwake kupata allergy.
🏮Makosa tunayofanya katika kumuanzishia mtoto chakula afikapo miezi 6
🍲kumpa mtoto vyakula visivyo na virutubisho bora.
🍲kuwahi sana au kuchelewa sana kumuamzishia mtoto chakula kingine.
🍲mtoto kupewa chakula kodogo sana au mara chache sana na kupelekea kushindwa kutimiza mahitaji yake ya siku kwa ajili ya ukuaji.
🏮Muda gani bora kumuanzishia mtoto chakula?
🍲Mtoto anyonyeshwe tu maziwa ya mama tangu anazaliwa hadi afikishapo miezi sita bila kumpa hata maji, maziwa ya mama ni bora, yana kinga na yanatosha kumfikishia mtoto mahitaji yote ya lishe ya siku.
🍲Anapofikisha miezi sita, ndio mtoto aanze kupewa vyakula vingine, maana muda huu mfumo wake wa ukuaji na mahitaji yake huongezeka na maziwa ya mama pekee hayamtoshelezi, hivyo mtoto apewe chakula na kunyonyeshwa pia.
🏮Chakula kipi ni bora kumpa mtoto muda huu?
🍲 Vyenye virutubisho muhimu.
🍲Visivyo na viungo vingi.
🍲Rahisi kuliwa na mtoto.
🍲Vinavyopendelewa na mtoto.
🍲Vinavyopatikana kwa urahisi na unafuu.
🏮 Mfano wa vyakula sahihi mtoto kupewa.
🍲 Maziwa ya mama, huleta joto na virutubisho bora kwa kiasi kikubwa mpaka mtoto afikapo miezi 23.
🍲Nafaka hutia nguvu, kumpa mtoto baadhi ya protini na vitamini, mfano; mchele, mtama, mahindi, mihogo, viazi
🍲Vitokanavyo na wanyama, huleta protini, madini na vitamini mfano; maini, nyama, samaki, mayai.
🍲Maziwa, huleta protini, nguvu, vitamini ,madini mfano;mtindi na maziwa
🍲 Mboga za majani na za rangi ya chungwa, huleta vitamini, mfano; spinach, karoti, maboga, viazi vitamu vya lishe.
🍲Jamii ya kunde, huleta protini kiasi, mfano;choroko, njegere, mharage
🍲Mafuta hutia joto, mfano; siagi
🍲Mbegu, huleta nguvu, mfano; siagi ya karanga, mbegu za maboga, tikiti.
🏮 Unamuanzishiaje mtoto lishe ya chakula kipya?
🍲Mpe mtoto chakula aina moja kisicho na viungo, kurahisisha upokeaji wake.
🍲Ruka siku saba na umuanzishie aina ingine ya chakula, kisicho na viungo.
🍲Mpe mtoto vijiko viwili mpaka vitatu vya chakula kipya kwa siku za mwanzo ili kurahisisha upokeaji.
🍲Mtazame mtoto kwa ukaribu kupata matokeo baada ya kumpa chakula
Angalia vipele, kukohoa na kupiga chafya, au kuharisha. ni dalili za allergy.
🍲Pia kurahisisha kujua tabia ya kula ya mtoto ( mvivu au mlaji kupitiliza)
🏮 Kanuni bora za lishe ya mtoto akiwa wa miezi sita hadi miaka miwili.
🍲Zingatia usafi katika uandaaji na ulishaji.
🍲Usichanganye chakula kibichi na kilichopikwa wakati wa kuandaa, kulisha au kutunza.
🍲Ivisha vizuri
🍲Tunza chakula katika joto salama.
🍲Tumia maji safi na salama.
🍲Mlishe mtoto kwa upendo ukimuongelesha na kumhimiza kujitahidi kula.
🍲Zuia usumbufu katika mazingira yanayozunguka sehemu ya kumlishia mtoto.
Hii husaidia watoto ambao ni wavivu kula.
🍲Ongeza kiasi cha chakula kidogo kidogo kadri mtoto akuavyo.
🍲Mlishe mtoto aina mbali mbali za vyakula kutimiza mahitaji muhimu ya virutubisho.
🍲Tumia virutubisho vilivyoandaliwa tayari kwa kitaalamu. Kulingana na mahitaji na upatikanaji.
🍲Kipindi mtoto aumwapo;
💉Ongeza kiasi cha vyakula vya kimiminika.
💉Mnyonyeshe zaidi na umhimize mtoto kwa upendo kula vyakula laini na apendavyo.
💉Mpe mtoto vyakula kiasi kiasi mara nyingi zaidi kumsaidia kuweza kula chakula cha kumtosha bila kuchoka.
🏮 Je ni kiasi gani cha chakula kinatosha kukamilisha mahitaji ya virutubisho kwa mtoto ?
🏮 Miezi 6
🍲uji laini au chakula kilichopondwa.
🍲Mtoto apewe milo 2 kwa siku.
🍲kwa kila mlo vijiko viwili mpaka vitatu vya chakula kwa siku pamoja na kunyonya maziwa ya mama.
🍲kama mtoto hanyonyi vya kutosha hakikisha anapata maziwa yalioandaliwa vizuri kwa ujazo wa nusu lita kwa siku.
🏮 Miezi 7 hadi 8
🍲Mtoto apewe chakula kilicho pondwa au uji
🍲Ale mara 3 kwa siku
🍲Apewe sehemu mbili ya tatu kwenye kikombe chenye ujazo wa 250mls (robo lita) kwa kila mlo.
🍲Aendelee kunyonya au maziwa yalioandaliwa nusu lita kwa siku.
🏮 Miezi 9 hadi 11
🍲vyakula vilivyopondwa au kukatwa vipande vidogo vidogo na ambavyo mtoto anaweza kuokota mwenyewe.
🍲apewe milo 3 kwa siku na mlo 1 wa kati.
🍲Apewe kiasi cha robo tatu ya kikombe chenye ujazo wa 250mls (robo lita) kila mlo.
🍲Aendelee kunyonya au maziwa yalioandaliwa nusu lita kwa siku.
🏮 Miezi 12 hadi 24
🍲Vyakula vya kawaida vya familia.
🍲vilivyopondwa au vilivyokatwa vipande kama vitahitajika mtoto apewe.
🍲Ale mara 3 kwa siku na milo ya kati mara 2.
🍲Apewe kiasi cha ujazo wa kikombe robo lita kwa kila mlo.
🏮 MUHIMU
🍲KUMPELEKA MTOTO CLINIKI KWA AJILI YA VIPIMO NA CHANJO KAMA UTAVYOELEKEZWA NA KITUO CHA AFYA KARIBU YAKO.
🍲MAJI SAFI NA SALAMA YA KUNYWA MTOTO APEWE KULINGANA NA ATAVYOHITAJI.
By Sylvia Senkoro
AfyaLishe tz
0754031039/0655568468
afyalishetz@gmail.com
Nina jarida langu nimeliandaa linalo husu afya na chakula kwa mtoto je? Naweza shea nanyi?
ReplyDeleteNdio
DeleteShare nasi please
DeleteIkiwezekana andaa telgram group tujifunze vizuriiii
ReplyDeleteKuna athari gani endapo moto anaanza uko kwa miezi 4 au 5?
ReplyDeleteAsante sana walau nimepata mwanga
ReplyDelete