UANDAAJI SAHIHI WA MAZIWA YA NG'OMBE KWA MTOTO MIEZI 6 HADI MWAKA.
🏮Mfumo wa kumeng'enya chakula kwa mtoto wa miezi 6 hadi mwaka bado haupo na uwezo wa kumengenya virutubisho vilivyopo kwenye maziwa ya ng'ombe
🏮usipoyataarisha maziwa hayo inavyotakiwa kabla ya kumpa mtoto unaweza kumsababishia;
🍼maumivu ya tumbo sababu ya kujaa gesi (kiwango kikubwa cha casein aina ya protini zilizopo kwenye maziwa ya ng'ombe )
🍼chembe za kupata allergy kutokana na (whey) aina za protini zilizopo kwenye maziwa hayo ambavyo uwiano wake ni mkubwa kuzidi uwezo wa umeng'enyaji chakula kwa mtoto.
🍼🍼🍼🍼🍼🍼🍼
Jinsi ya kutayarisha maziwa ya ng'ombe kwa kumpa mtoto (miezi 6 hadi mwaka)
🏮 Mahitaji
Maziwa ya ng'ombe
Maji salama
Sukari
🏮 Uwiano
Ili kupata 400mls za mchanganyiko.
🍼Maziwa ya ng'ombe- Robo lita 250mls
🍼Maji salama- Nusu ya robo 125 mls
🍼Sukari - vijiko 2 na nusu vya chakula 25g
🏮 Upikaji
🍼Changanya mchanganyiko wako kwa uwiano hapo juu.
🍼Chemsha mchanganyiko huo, hakikisha maziwa yameiva.
🏮 Kiasi cha kupewa mtoto
🍼Mtoto apewe mls 500 kwa siku pamoja na chakula kingine.
By Sylvia Senkoro
AfyaLishe Tz
Contacts: 0754031039/0655568468
sylsenkoro@gmail.com
afyalishetz@gmail.com
Asante sana Mtaalamu wetu Sylvia Senkoro wengi hautjui hili la uchanganyaji wa maziwa ya ngombe kwaajili ya kumuandalia mtoto wa anaeanza kula
ReplyDeleteAsante dada Sylvia
ReplyDeleteAhsante sana madam, je kuna ulazima wa kuweka sukar?
ReplyDeleteThank you sanaaaa mwanangu kwenye kula anasumbua sana hivyo nilikuwa nafikiria jinsi ya kumpa maziwa ya ng'ombe..Nashukuru kwa somo.
ReplyDeleteThenk your
ReplyDelete