Skip to main content
""Kwa msaaada zaidi wasiliana nasi kwa namba zifuatazo 0754031039/0655568468 AfyaLishe Tz kwa ajili yako""

COUNSELLING DESK

COUNSELLING DESK
Tumia huduma yetu ya ushauri, na kujadiliana. Kwa matatizo ya kifamilia, kibiashara, kielimu, kiafya, mahusiano na mfumo mzima wa maisha wasiliana nasi kwa 0754031039 au 0655568468

DHIBITI MSONGO NA PARACHICHI/ CONTROL STRESS WITH AVOCADO


DHIBITI MSONGO NA PARACHICHI/ CONTROL STRESS WITH AVOCADO.
ENGLISH VERSION
If you are looking for a delicious and nutritious way to lower your stress levels, look no further than an avocado. B vitamins are heavily involved in regulating our metabolism and hormone levels, both of which are impacted by social anxiety disorder.
A deficiency in B vitamins can often lead to mood swings and energy surges, and higher levels of stress hormones in the body. Avocados are packed with B vitamins and can help give you back your anxiety-free life. Avocados can also impact circulatory and blood pressure issues, which will help keep you calm.

SWAHILI VERSION.
Ikiwa unatafuta njia bora ya kupunguza kiwango cha msongo wa mawazo, usiende mbali, tumia parachichi. Vitamini B vinahusika sana katika kusimamia kazi za kimetaboliki mwilini na udhubiti wa viwango vya homoni, ambavyo vyote vinaathiriwa na matatizo ya kijamii na msongo. Ukosefu wa vitamini B huweza kusababisha mpingano wa kihisia, upungufu wa nishati, na viwango vya juu vya homoni ziletazo msongo na uchovu katika mwili. Parachichi imejaa viwango vya Vitamini B, hivyo kuweza kudhibiti msongo. Pia parachichi  huweza kudhibiti mzunguko na shinikizo la damu, ambayo pia itasaidia kuuweka mwili katika hali ya utulivu.

AfyaLishe Tz
Sylvia Senkoro
afyalishetz@gmail.com

0754031039

Comments

  1. parachichi hill naliandaaje??
    nalitumia kama kawaida mfano katika chakula? au vipi


    maternus 4rm Mbeya Tz

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari martenus kutoka mbeya, hakuna njia maalumu sana ya kuandaa parachichi hili, unaweza kutumia kama tunda au juice .

      Lakini zingatia kuna baadhi ya vyakula vikichanganywa na vingine huzuia unyonywaji wa virutubisho vyake mwilini.

      Hivyo tunashauri pata matunda nusu saa kabla ya kupata mlo wako.

      Karibu sana.

      Delete

Post a Comment

NEWS

NEWS
Kula lishe bora kuepuka hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa.

Chagua afya leo.

EXCLUSIVE BREASTFEEDING

EXCLUSIVE BREASTFEEDING
Make sure your child gets breastfed exclussively for the first six months, the child shouod not be fed anything else not even water. This adds up to the child's immunity and increase chencea of proper development.

Popular posts from this blog

UANDAAJI WA LISHE YA UJI UNAOTAKIWA KWA MTOTO MIEZI SITA NA KUENDELEA

UANDAAJI WA LISHE YA UJI UNAOTAKIWA KWA MTOTO MIEZI SITA NA KUENDELEA Tumekua na tamaduni ya kuandaa uji wa lishe ya mtoto bila kufuata kanuni za uandaaji bora. Madhara ya uji usio bora

UANDAAJI MAZIWA YA SOYA UKIWA NYUMBANI

Maziwa ya Soya Aina hii ni maarufu pia, na kwa kuwa yanatokana na mimea, maziwa haya hana cholesterol ( lehemu) - tofauti na maziwa ya kawaida. Maziwa ya Soya pia yana kiwango cha chini cha kalori kuliko maziwa ya ng'ombe, yana kalori takribani 130 kwa kila kikombe. Hakuna lactose  katika maziwa haya, aina ya protini inayoleta sana gesi tumboni, hivyo huyafanya kuwa mbadala muhimu kwa watu ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa kushindwa kuvumilia lactose (lactose intolerance) katika mfumo wao wa umeng'enyaji, pamoja na watu wasiotumia bidhaa zitokanazo na wanyama pia (vegeterians) sababu haitoki kwa wanyama.  Soya ni mboga nzuri sana, na maziwa yanayotokana na jamii hii yana utajiri wa potasiamu, protini na kalsiamu ikiwa mtengenezaji atayaimarisha na madini. Pia ni chanzo kikubwa cha vitamini A na vitamini B12, ambayo haipo katika aina nyingine za maziwa. Maziwa ya Soya hutoa kiwango cha juu cha protini, pia ni bora kwa watu ambao wanajaribu kudhibiti uzito wao au kupu...

ONGEZA UWEZO WAKO WA KUMNYONYESHA MTOTO

ONGEZA UWEZO WAKO WA KUMNYONYESHA MTOTO Mtoto anyonye maziwa ya mama tu hadi ayakapotimiza Miezi sita. Utakua umemuepushia magonjwa na hatari zingine nyingi tu. Kama mama hana maziwa ya kutosha mtoto pia anaweza kupewa formula milk ila ni pale tu mama akiwa maefariki au akiwa na tatizo kama hilo la maziwa kuto tosha. Lakini ni muhimu mama kukazana kuhakikisha maziwa yanatosha ili mtoto awe katika hali salama na afya zaidi. Fahamu vitu vifuatavyo vimesaidia wengine 🍵Maziwa ya mama yametengenezwa na vtu vi3 vya muhimu *maji ambayo ndio mengi *Protein and *Fats 🍵 ni muhimu sana kufahamu kwamba  kutoka kwa  Maziwa kunahitaji activity ya hormones/ homoni ziwe stimulated, na kinachostimulate ni mtoto kunyonya au kuvuta chuchu Hivyo mtoto anavovuta au kunyonya chuchu ya mama yake ndivo hormones za kutengeneza  maziwa zinavozalishwa zaidi, hivyo kuleta matokeo chanya katika unyonyeshaji. Mama asikate tamaa kumueka mtoto kwenye chuchu hata kama maziwa hayat...
""AHSANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU, KARIBU TENA/ THANK YOU FOR VISITING OUR BLOG, YOU ARE WELCOME""