Kisaikolojia.
Binadamu huzaliwa akiwa blank hana kitu akilini mwake, Lakini kadri akuavyo mazingira yanayomzunguka yanamjaza akili.
Moja ya tabia ni kuwapa wengine maumivu ya moyo bila kujali matokeo wala hali ya mtendewa.
Hii inaweza kutafsitiwa hivi,
Binadamu akipitia kitu chochote cha kumuumiza au kama kuna kitu alikiona huko nyuma na kikamfanya atumie nguvu nyingi kukivumilia basi hiyo hubaki kama resistance/ *SUGU* ya moyo wake kutokujali vitu au watu.
Vyote vitavyopita ataona ni kawaida na wala hatawaza italeta madhara gani.
Akili yake itaona kua kila mtu yuko hivo na maisha ndivo yalivo.
Watu wa aina hii huwa wa kipekee, hutunza siri na hawi mtu wa kujichanganya na watu katika story za kugusa maisha yao. Yeye huisi kila mtu ni kama yeye. Na hakuna haja ya kuingilia ya wengine wala kuingiliwa yeye katika mambo yake.
Mtu wa hivi anaweza kupona akipata experience za watu wengine.
Au akipata madhara kwa aliyoyafanya.
Ila bila hivo ataona ni sawa tu.
Na ndio mana siku atakua vizuri na siku atatibuka ni mtu wa moods tu.
Ila sio mbaya.
Ukifahamu jinsi ya kuishi na mtu huyu, unaweza msaidia na anaweza akapona na kuwa mtu mwema na wa upendo.
Counselling Desk/ Dawati la Ushauri
By Sylvia Senkoro
AfyaLishe TZ
0754031039
Karibu kwa ushauri Huduma zetu ni bure
Comments
Post a Comment