```●Nina furaha kukwaambia kwamba bado hujachelewa kuweka lengo jipya na kuamua kulifanyia kazi katika safari inayoendelea katika maishs yako.
●Zifuatazo ni baadhi ya mifumo ya maisha inayoweza kukufanya ufanikishe malengo yako muhimu katika maisha.```
1. Ona kushindwa kama mwanzo wa kitu kipya
2. Mshirikishe Mungu kabla ya jambo lolote
3. Andaa nguo nadhifu ya kuvaa kesho kabla hujalala, amka mapema, tandika kitanda chako na usisahau kujali afya yako.
4. Tafuta amani na yaliyopita kabla hayajakutesa
5. Weka malengo makubwa lakini anza na dogo lililo ndani ya uwezo wako
6. Usiwekee labda katika vitu bali pima kilakitu
7. Usijifananishe na watu
8. Andika malengo yako
9. Panga mipango ya namna utatimiza malengo yako
10. Tafuta hekima na maarifa juu ya mambo mbali mbali hasa lile unslotazamia kufanya.
11. Fanya kazi yenye manufaa kwako
12. Tumia kidogo zaidi ya unacho ingiza
13. Wekeza katika mawazo yako
14. Kopa kwa manufaa
15. Epuka wapoteza muda
16. Tunza mahusiano yenye manufaa
17. Kutana na watu wapya waliokuzidi hatua fulani ya kimaendeleo.
18. Ni vizuri kuwafahamu wakosoaji wako na fahamu wanachokosoa na ukifanyie kazi kama kina mantiki.
19. Baki katika muelekeo wako
20. Chukua hatua baada ya kupima manufaa
21. Jifunze kwa unaowatamani
22. Chukua hatua hata kama inaogopesha
23. Tafuta maana yenye kutia moyo katika jambo umalofanya
24. Fanya kitu kimoja kwa wakati.
25. Kifanye taratibu kwa ufanisi na kwa ufasaha.
26. Fanya zaid ya unavyotegemewa
27. Kuwa mtu wa watu na Fundisha watu unachojua
28. Tengeneza tabia ya kuwa wa kushukuru
29. Weka muda wa kuwa karibu na familia yako na kuwasikiliza
30. Usitafute maisha ukasahau kuishi, pumzika na jiburudishe kwa kiasi.
```●Kumbuka mawazo hasi au mawazo ya changamoto unazopitia hayana budi kuja ila ni wewe utakaeamua jinsi yatakavyotengeneza au haribu maisha yako.
●Nashauri kuwa na mtu wa karibu atakae kusaidia kubeba yako ya moyoni na kukutia moyo katika kila jambo, ni muhimu pia kuwa na mtaalamu wa ushauri (counselling specialist).```
Nashukuru kwa kupitia makala hii. Usisahau kusubscribe blog yangu ili uwe wa kwanza kupata mambo mapya kila siku.
By Resta Dietetics and Counselling
0754031039
```Karibu kwenye group letu, ujifunze lishe bora na mambo mengine mengi.```
https://chat.whatsapp.com/BFXj5ZT2p794abU8NAxJ0k
```Bonyeza link hapo juu kujiunga moja kwa moja.```
Comments
Post a Comment