Skip to main content
""Kwa msaaada zaidi wasiliana nasi kwa namba zifuatazo 0754031039/0655568468 AfyaLishe Tz kwa ajili yako""

COUNSELLING DESK

COUNSELLING DESK
Tumia huduma yetu ya ushauri, na kujadiliana. Kwa matatizo ya kifamilia, kibiashara, kielimu, kiafya, mahusiano na mfumo mzima wa maisha wasiliana nasi kwa 0754031039 au 0655568468

DODOSO LA KUMPOKEA MSAIDIZI WA KAZI ZA NYUMBANI


1. Majina kamili
2. Umri
3. Historia ya familia
4. Historia ya elimu
5. Historia ya Afya
6. Historia ya kazi na kwanini aliacha.
7. Ratiba yake ya siku
8. Kazi anazoweza kufanya
9. Kazi asizoweza kufanya na kwanini.
10. Aina ya vyakula asivyoweza kula na kwanini
11. Tambua Dini yake na imani zake.

*Zingatia*

●Baada ya kumdodosa dada, andika majibu yake na utumie hayo kumpangia majukumu yake na kanuni za kazi hapo kwako.

●Ni muhimu dada kupima afya yake pindi anapoingia kwako.

●Ni muhimu dada kuwa na barua ya utambulisho kutoka kijiji alipotoka iliyosainiwa ns yenye muhuri na saini ya mwenyekiti wake

●Ni muhimu dada kuja na kithibitisho cha wazazi au walezi wake kuridhia kufanya kazi hapo na uwe na mawasiliano nao.

●Ni muhimu kuweka wazi ratiba za likizo

●Ni muhimu kuweka wazi matumizi yatakayokua juu yako na atakayojitegemea

●Ni muhimu kumuandalia ratiba ya kazi itakayomuongoza kwa siku nzima.

●Ikiwezekana binti akaguliwe vitu alivyokuwa navyo anavyofika.

●Msisitize binti kuhusu usafi wa mwili wake na wa mazingira pamoja na chakula wakati anandaa

●Muajiri jitahidi kuishi na binti kwa upendo mpe motisha na kumpongeza anapofanya vizuri na kumuelekeza vizuri pale anapokosea ili ajifunze na si kumkaripia kila mara au hata kumpiga.

Angalizo: Iwapo utamnunulia binti zawadi mf. Nguo fanya kwa kiasi ili azoee, wengi hufurahi kuoitiliza na kutaka kurudi kwao kuringishia nguo zao na hii sio nzuri kwa muajiri

●Binti aelekezwe kupokea wageni na ndugu kwa ukarimu, lakini pia muajiri usiseme siri za familia au kumsema mtu wa familia mbele ya binti.

●kama una watoto waelekeze kujitegemea na kushiriki baadhi ya kazi, usijisahau ukaharibu watoto sababu wanafanyiwa kila kitu.

●Binti asaini mkataba unaoelekeza majukumu yake na kanuni za kazi na malipo yake.

●Binti asiaini kila anapopokea mshahara


```Lengo ni kujenga mipaka,heshima na usalama wa kazi.```

*Resta Dietetics &* *Counselling*
*0754031039*

```Karibu kwenye group letu, ujifunze lishe bora na mambo mengine mengi.```

https://chat.whatsapp.com/BFXj5ZT2p794abU8NAxJ0k

```Bonyeza link hapo juu kujiunga moja kwa moja.```

Comments

NEWS

NEWS
Kula lishe bora kuepuka hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa.

Chagua afya leo.

EXCLUSIVE BREASTFEEDING

EXCLUSIVE BREASTFEEDING
Make sure your child gets breastfed exclussively for the first six months, the child shouod not be fed anything else not even water. This adds up to the child's immunity and increase chencea of proper development.

Popular posts from this blog

UANDAAJI WA LISHE YA UJI UNAOTAKIWA KWA MTOTO MIEZI SITA NA KUENDELEA

UANDAAJI WA LISHE YA UJI UNAOTAKIWA KWA MTOTO MIEZI SITA NA KUENDELEA Tumekua na tamaduni ya kuandaa uji wa lishe ya mtoto bila kufuata kanuni za uandaaji bora. Madhara ya uji usio bora

KANUNI BORA ZA KUMUANZISHIA MTOTO CHAKULA AFIKAPO MIEZI SITA

KANUNI BORA ZA KUMUANZISHIA MTOTO CHAKULA AFIKAPO MIEZI SITA 🏮 Kwanini nianze kumpa mtoto wa miezi 6 chakula kingine? 🍲Mtoto wa miezi sita ameanza kuwa na mahitaji ya virutubishi  kwa wingi zaidi ya anavyopata kutoka kwenye maziwa ya mama.

ONGEZA UWEZO WAKO WA KUMNYONYESHA MTOTO

ONGEZA UWEZO WAKO WA KUMNYONYESHA MTOTO Mtoto anyonye maziwa ya mama tu hadi ayakapotimiza Miezi sita. Utakua umemuepushia magonjwa na hatari zingine nyingi tu. Kama mama hana maziwa ya kutosha mtoto pia anaweza kupewa formula milk ila ni pale tu mama akiwa maefariki au akiwa na tatizo kama hilo la maziwa kuto tosha. Lakini ni muhimu mama kukazana kuhakikisha maziwa yanatosha ili mtoto awe katika hali salama na afya zaidi. Fahamu vitu vifuatavyo vimesaidia wengine 🍵Maziwa ya mama yametengenezwa na vtu vi3 vya muhimu *maji ambayo ndio mengi *Protein and *Fats 🍵 ni muhimu sana kufahamu kwamba  kutoka kwa  Maziwa kunahitaji activity ya hormones/ homoni ziwe stimulated, na kinachostimulate ni mtoto kunyonya au kuvuta chuchu Hivyo mtoto anavovuta au kunyonya chuchu ya mama yake ndivo hormones za kutengeneza  maziwa zinavozalishwa zaidi, hivyo kuleta matokeo chanya katika unyonyeshaji. Mama asikate tamaa kumueka mtoto kwenye chuchu hata kama maziwa hayatoki auni macha
""AHSANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU, KARIBU TENA/ THANK YOU FOR VISITING OUR BLOG, YOU ARE WELCOME""