Wengi wetu angalau tumepata neema ya kusoma chekechea ama basi hata darasa la kwanza.
Hiki huwa kipindi muhimu kwetu maana unaanza kuingia katika jamii, wale uliowazoea nyumbani sio utakaowakuta huko shule, namaanisha unakutana na watu wasiokuhusu kwa asilimia 100.
Lakini kadri unavyoishi nao unajikuta mnafahamiana kisha mtakutana kwenye michezo kisha kuna kikundi cha watu wawili watatu ambacho utajikuta umeingia bila mpango ama kutambua ila basi tu ndio mmeendana na mnakua marafiki wa karibu (best friends) kuanzia hapo.
Hii ndio stage kubwa ya mwanzo utaanza nahusiano. Ila utakubaliana na mimi pindi utakapohamia level ingine ya kielimu, wale wa nyuma utawasahau kabisa na ni wachache huweza kumaintain urafiki huu hadi utuuzima au hata mawasiliano tu.
Kwanini nimetumia mfano huo?
Hii ni sababu hata na utu uzima huu tumepoteza mahusiano ya wale watu wa muhimu kwetu wanaotuhusu asilimia 100 na kuingia katika kujali mahusiano na watu wasiotuhusu kwa asilimia 100.
Unaweza ukawa hujaelewa bado ninachojaribu kukwambia.
Jiulize kati ya shosti yako mliokutana group la whatsaap au yule jamaa uliokutana nae katika bar jioni ukipumzika na yule wa karibu yako unaeishi nae nyumba moja yupi unampa nafasi na je ikitokea una tatizo ni nani atakupa nafasi???
Nafkiri unajiuliza na kuna majibu umepata
Ndugu yangu katika maisha Jifunze kumpa kila mtu umuhimu kulingana na umuhimu atakaokupa wewe kipindi upo katika shida ya ndani.
Wanaume wanamuona bar maid ah mchepuko ni wa muhimu zaidi au yule msela wake ni muhimu zaidi kuliko mke wake wa ndani.
Mpaka kipindi mtu anakufa ndio mke wake anajua kua kumbe kuna nyumba iko sehemu flani au kuna kiwanja kipo sehemu fulani. Familia inaingia mafarakano na watoto ndio wanaopata tabu.
Wanawake wengi wamepoteza ndoa zao kwa ujinga wa mashosti wa facebook, whatsapp, instagram na vibarazani, wanatumia experience za marafiki kuhimili au kutatua changamoto katika familia yake na kusahsu kua mume wa shosti ni engineer na wake ni daktari, hawa watu wapo mazingira tofauti kabisa halafu wote unataka kutumia formula moja kuishi nao!!!, unashangaa kama alikua anarudi saa tatu usiku ndio anarudi asubuhi. Nani wa kumlaumu?
Vijana wengi wamejikuta kwenye mahusiano wasiyoyastahili ya baadae unakua mzigo mzito na huwez kuutua tena maana ukiangalia unaona umepoteza muda, na kwa umri wako sasa hivi unawaza utaanzaje upya.
Nani wa kukaumiwa???
Hakikisha unachagua kwa makini jinsi ya kutumia muda wako katika mahusiano unayokutana nayo.
Sio lazima muwe karibu sana, sio lazima ajue siri zako, wacha Mungu azijue siri zako maana ndipo pekee itabaki kua siri na utapata jawabu la kudumu.
Usiruhusu mahusiano yasiyo na faida yakupotezee muda wako na mahusiano yako yakudumu.
Usiingie katika mahusiano kama mtoto alieanza kindergatten au la kwanza. Ukashangaa kipindi cha shida wale wa nyumbani wote umewapoteza na yule uliemuona wa karibu yupo busy na watu wanaomuhusu kwa asilimia 100. Katika hatua hii ndio utagundua kwamba sio kila muda kuna second chance!!!
By Resta Dietetics & Counselling
0754031039
```Karibu kwenye group letu, ujifunze lishe bora na mambo mengine mengi.```
https://chat.whatsapp.com/BFXj5ZT2p794abU8NAxJ0k
```Bonyeza link hapo juu kujiunga moja kwa moja.```
Comments
Post a Comment