MAKALA YA 102
http://afyalishetz.blogspot.com/2019/07/sayansi-nyuma-ya-detox-na-kupunguza.html
N:B Asilimia 60 ya uzito ulionao ni maji, hivyo kadri unavyopoteza maji ndivyo unapoteza uzito.
Mf: Mtu mwenye kilo kg100 akifanikiwa kupoteza lita 10 za maji mwilini mwake, atakua amefanikiwa kupunguza kilo kg14 za uzito wake.
Katika dunia ya leo kila mtu anahitaji kuwa na mwili unaovutia na kupendeza. Kwa bahati mbaya wengi tunatamani hili bila ya kulifanyia kazi.
Kutokana na tamaa hii tuliyonayo basi tumeibua ushawishi kwa wajasiriamali wengi kuanza biashara ya uuzaji wa detox tea
(chai za kusafisha na kupunguza mwili)
Nimeandika ili kwa wale tusio fahamu tujifunze kitu.
```Tuanzie hapa
Nini maana ya detox?
Kwa lugha ya wenzetu Toxin ni sumu, hivyo Detox ni kitendo cha kuiondoa hiyo sumu.
Sasa kwa vile hapa naongelea zaidi mwili, naweza nikasema Detox ni kuondoa sumu mwilini.
Vinywaji vya Detox huwa na *Antioxidants*, kwa lugha rahisi tunaweza kusema ni *Viua sumu*.
Viungo kama vitunguu swaumu, mchai chai, karafuu, hata matunda pia huwa na hivi vitu viitwavyo viua sumu, ambavyo hutumika kusafisha mwili na kuondoa sumu, kwa njia ya kurahisisha umeng'enyaji wa chakula hivyo mtu anaweza kupata choo kizuri kila siku ambayo ni njia nzuri ya kuzuia sumu zisifyonzwe mwilini na kutoka kwa njia ya kupata choo.
Kama umenielewa naweza nikakwambia kwamba, katika mauzo ya hizi detox tea, wauzaji watakwambia:
'' Mteja wangu hii detox usipokula vizur na kufanya mazoezi hautapata matokeo mazuri, hivyo kua makini''
Hii humfanya mteja alietumia pesa yake nyingi, kujitahidi kula vizur na kufanya zoezi pamoja na kutumia Detox yake huku akiamini atapungua na kweli ndani ya wiki ama wiki mbili mtu huanza kuona matokeo chanya.
Pia wauzaji wengine huenda zaidi na kusema kwamba:
''ukiacha kutumia hii detox utarudia tena unene na kitambi kitarudi kama kilivyokua''
```Jiulize swali.........```
Je kilichompunguza huyu mtu ni detox tea au kula vizur na mazoezi?
```JE KUNA MADHARA YOYOTE YA KUTUMIA DETOX```
Detox nyingi huwa hazina kemikali mbaya, huwa ni bidhaa mbali mbali za asili mfano, mchai chai, karafuu, n.k ambavyo huwa havina madhara.
▪Lakini ili kuongeza ufanisi wake wa kufanya kazi kwa haraka kuna kemikali huwa zinaongezwa.
Ndio pale utasikia muuzaji anakwambia:
"Detox hii ukitumia hata ukila vipi ni lazima tu utapungua maana ina flush kila kitu"
▪Mara nyingi Detox huweza kuwa na kemikali za kukufanya kuwa active au mchangamfu na mwenye nguvu kwa muda bila kusikia njaa.
▪Pia inaweza kukufanya ukaharisha sana sababu ya kuwa na laxatives
(madawa yanayotumika kutibu constipation).
Na hii hupelekea kupunguza mwili kwa kupoteza maji mwilini.
Kwa mantiki iliyoelezwa mwanzoni kabisa mwa nakala hii, Matumizi ya Detox hupunguza zaidi maji (water weight) na sio sumu kama inavotangazwa.
Kadri unavyopoteza maji ndivyo unavyopoteza uzito
▪Kutokana na hii, kuharisha kupitiliza kunaweza pia kusababisha(electrolyte imbalance), kupotezwa kwa madini mengi ya chumvi chumvi ( sodium chloride) ambazo zinazotumika kusawazisha maji ya mwilini na kufanikisha baadhi ya shughuli za figo.
▪Pia utendaji wa misuli huweza kufifishwa, na hii ni hatari kwasababu inaweza kupooza ufanisi wa misuli ya kawaida na ukawa kama huna control na movement za misuli yako lakini pia misuli ya kwenye moyo na kusababisha mapigo ya moyo kutokua sawa.
▪Madawa haya pia yakitumika muda mrefu yanaweza kuathiri ( Bowel movements) utendaji wa utumbo katika kumeng'enya chakula na kusababisha uwe unategemea hizo laxatives ili kupata choo vizur na si kwa njia ya kawaida tena yaani bila matumizi ya madawa.
▪Pia unaweza ukapata matatizo ya kichefu chefu, tumbo kujaa gesi na maumivu ya tumbo.
▪Ukosefu wa usingizi tulivu kwasababu baadhi ya Detox huwa na caffein na ikizidi kiwango kwa siku huweza sababisha ukosefu wa usingizi mtulivu.
▪Pia kama upo kwenye dozi tofauti baadhi ya detox zinaweza kuathiri utendaji sahihi wa dozi hizo, maana zinaweza kutoka mwilini kwa njia ya mkojo au kuharisha kabla hata hazijafanya kazi yake mwilini.
USHAURI WETU
Matumizi ya Detox yawe kwa kiasi, pia hakikisha Detox unazotumia zimeruhusiwa na kupitishwa kwa matumizi na TMDA/ TBS au shirika zingine kwa nchi jirani.
Njia sahihi ya kupata mwili bora ni kwa kuzingatia ulaji sahihi ( healthy weight loss Diets) na ufanyaji wa mazoezi.
```Karibu kwa ushauri zaidi kuhusu lishe bora za watoto na rika zote, diet za kudhibiti uzito, kisukari, presha n.k .```
_Imeandikwa na ;_
_Sylvia Senkoro_
Resta Dietetics & Counselling
0754031039
Cc: CHOICELINE Co. Ltd
Comments
Post a Comment