Skip to main content
""Kwa msaaada zaidi wasiliana nasi kwa namba zifuatazo 0754031039/0655568468 AfyaLishe Tz kwa ajili yako""

COUNSELLING DESK

COUNSELLING DESK
Tumia huduma yetu ya ushauri, na kujadiliana. Kwa matatizo ya kifamilia, kibiashara, kielimu, kiafya, mahusiano na mfumo mzima wa maisha wasiliana nasi kwa 0754031039 au 0655568468

SOMO LA 9 NA RESTA ( SIKU 1000 ZA MTOTO)

 ``
LISHE YA MAMA MJAMZITO```

Matatizo yanayotokana na upungufu wa Iodini (IDD)

 _Goitre_
kuzidi kwa eneo la shingo kutokana na kuathirika kwa tezi ya thairoidi.

_Hyothyothyism_
Ngozi kavu, uzito kuongezeka, uso kuvimba.

_Hyperthyroidism_
Mapigo ya moyo kwenda haraka na kupoteza uzito kutokana na tezi kuathirika.

_Cretinism_
Matatizo ya akili, matatizo katika maendeleo ya kimwili, hali ya Udumavu na ulegevu kwa mama mjamzito kakili na kimwili.
Mf. Kusahau sahau, mama anaweza akawaza anataka afanye hiki lakini mwili wake umefanya vingine kabisa. Au hata mtu kua taratibu katika kufanya mambo yake hata kuamua.

MAJI NA VYAKULA VYENHE NYUZI HUKAMILISHA LISHE BORA KWA MAMA MJAMZITO


I. _Nyuzi nyuzi za vyakula (fibers)_

Fibers (nyuzi) za vyakula ni sehemu ya chakula ambayo haviwezi kuvunjika vyote na pia hua vichochezi vya umengenyaji  (enzymes) katika utumbo mwilini mwa binadamu.

_Chakula chenye jamii ya nyuzi (fiber) husaidia kuboresha kazi za utumbo hivyo inaweza kuzuia na kutibu kuvimbiwa na kuepusha choo kigumu._

Jamii hii ya vyakula ikihusishwa kwenye mlo imehusishwa katika kuzuia kansa ya utumbo mkubwa.

*Vyanzo vya vyakula vya nyuzi nyuzi ni pamoja na matunda na mboga mboga, nafaka zisizohifadhiwa na jamii ya mikunde.*

II. _Maji_

Maji ni sehemu muhimu ya chakula.

_Katika mwili, maji ni muhimu kwa usafirishaji wa virutubisho na kuondoa taka._

_Maji husaidia katika shughuli za kimetaboliki kwenye seli na kulaiisha sehemu za mwili zinazosonga na kusaidia katika kudhibiti joto la mwili._

Wakati wa ujauzito, mahitaji ya maji yanaongezeka hadi lita 3 kwa siku, hii ni kwa sababu ya
▪Kuongezeka kwa kiasi cha damu ya mama,
▪Kudhibiti wa joto la mwili, maana joto la mwili huongezeka,
▪Kuzalishaji wa maji yanayozunguka mfuko wa uzazi (placenta) kwa ajili ya kumlinda  mtoto.
▪Kusaidia kuzuia choo kigumu kwa mama mjamzito
▪Kupunguza hatari ya kupata maambukizi kwa ya njia ya mkojo.

Familia kwa ujumla na wazazi watarajiwa  wazingatie mahitaji ya virutubishi hivi katika uandaaji wa chakula cha mama mjamzito.

By Resta Dietetics & Counselling
0754031039

Comments

NEWS

NEWS
Kula lishe bora kuepuka hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa.

Chagua afya leo.

EXCLUSIVE BREASTFEEDING

EXCLUSIVE BREASTFEEDING
Make sure your child gets breastfed exclussively for the first six months, the child shouod not be fed anything else not even water. This adds up to the child's immunity and increase chencea of proper development.

Popular posts from this blog

UANDAAJI WA LISHE YA UJI UNAOTAKIWA KWA MTOTO MIEZI SITA NA KUENDELEA

UANDAAJI WA LISHE YA UJI UNAOTAKIWA KWA MTOTO MIEZI SITA NA KUENDELEA Tumekua na tamaduni ya kuandaa uji wa lishe ya mtoto bila kufuata kanuni za uandaaji bora. Madhara ya uji usio bora

UANDAAJI MAZIWA YA SOYA UKIWA NYUMBANI

Maziwa ya Soya Aina hii ni maarufu pia, na kwa kuwa yanatokana na mimea, maziwa haya hana cholesterol ( lehemu) - tofauti na maziwa ya kawaida. Maziwa ya Soya pia yana kiwango cha chini cha kalori kuliko maziwa ya ng'ombe, yana kalori takribani 130 kwa kila kikombe. Hakuna lactose  katika maziwa haya, aina ya protini inayoleta sana gesi tumboni, hivyo huyafanya kuwa mbadala muhimu kwa watu ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa kushindwa kuvumilia lactose (lactose intolerance) katika mfumo wao wa umeng'enyaji, pamoja na watu wasiotumia bidhaa zitokanazo na wanyama pia (vegeterians) sababu haitoki kwa wanyama.  Soya ni mboga nzuri sana, na maziwa yanayotokana na jamii hii yana utajiri wa potasiamu, protini na kalsiamu ikiwa mtengenezaji atayaimarisha na madini. Pia ni chanzo kikubwa cha vitamini A na vitamini B12, ambayo haipo katika aina nyingine za maziwa. Maziwa ya Soya hutoa kiwango cha juu cha protini, pia ni bora kwa watu ambao wanajaribu kudhibiti uzito wao au kupu...

ONGEZA UWEZO WAKO WA KUMNYONYESHA MTOTO

ONGEZA UWEZO WAKO WA KUMNYONYESHA MTOTO Mtoto anyonye maziwa ya mama tu hadi ayakapotimiza Miezi sita. Utakua umemuepushia magonjwa na hatari zingine nyingi tu. Kama mama hana maziwa ya kutosha mtoto pia anaweza kupewa formula milk ila ni pale tu mama akiwa maefariki au akiwa na tatizo kama hilo la maziwa kuto tosha. Lakini ni muhimu mama kukazana kuhakikisha maziwa yanatosha ili mtoto awe katika hali salama na afya zaidi. Fahamu vitu vifuatavyo vimesaidia wengine 🍵Maziwa ya mama yametengenezwa na vtu vi3 vya muhimu *maji ambayo ndio mengi *Protein and *Fats 🍵 ni muhimu sana kufahamu kwamba  kutoka kwa  Maziwa kunahitaji activity ya hormones/ homoni ziwe stimulated, na kinachostimulate ni mtoto kunyonya au kuvuta chuchu Hivyo mtoto anavovuta au kunyonya chuchu ya mama yake ndivo hormones za kutengeneza  maziwa zinavozalishwa zaidi, hivyo kuleta matokeo chanya katika unyonyeshaji. Mama asikate tamaa kumueka mtoto kwenye chuchu hata kama maziwa hayat...
""AHSANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU, KARIBU TENA/ THANK YOU FOR VISITING OUR BLOG, YOU ARE WELCOME""