MAKALA YA 102 http://afyalishetz.blogspot.com/2019/07/sayansi-nyuma-ya-detox-na-kupunguza.html N:B Asilimia 60 ya uzito ulionao ni maji, hivyo kadri unavyopoteza maji ndivyo unapoteza uzito. Mf: Mtu mwenye kilo kg100 akifanikiwa kupoteza lita 10 za maji mwilini mwake, atakua amefanikiwa kupunguza kilo kg14 za uzito wake. Katika dunia ya leo kila mtu anahitaji kuwa na mwili unaovutia na kupendeza. Kwa bahati mbaya wengi tunatamani hili bila ya kulifanyia kazi. Kutokana na tamaa hii tuliyonayo basi tumeibua ushawishi kwa wajasiriamali wengi kuanza biashara ya uuzaji wa detox tea (chai za kusafisha na kupunguza mwili) Nimeandika ili kwa wale tusio fahamu tujifunze kitu. ```Tuanzie hapa Nini maana ya detox? Kwa lugha ya wenzetu Toxin ni sumu, hivyo Detox ni kitendo cha kuiondoa hiyo sumu. Sasa kwa vile hapa naongelea zaidi mwili, naweza nikasema Detox ni kuondoa sumu mwilini. Vinywaji vya Detox huwa na *Antioxidants*, kwa lugha rahisi tunaweza kusema ni *Viua ...